Njia Rahisi ya Kupunguza Unene wa Mwili Ukiachana na Kufanya Mazoezi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kila mtu huwa anajiuliza ni jinsi gani ya kuondoa mafuta tumboni, iwe tumbo ni la kati au ni kitambi kimejitokeza. Kwa mwili mnene wenye mafuta mengi ni vigumu kuona matokeo mazuri ya kuridhisha kwa kufanya mazoezi pekee, maana asilimia hamsini ya mafuta mwilini huifadhiwa chini ya ngozi, na kiasi kingine kilicho baki huwa ndani ya misuli. Kufanya mazoezi ya mwili pekee hakuwezi kuondoa mafuta hayo mwilini. 

Mtu mnene akifanya mazoezi ya kuvuta tumbo hawezi kuona matokeo, hata kama akirudia mazoezi hayo mara mamia kwa siku, kitakachotokea ni kweli ataimalisha misuli yake ya tumbo ila  hatoweza kuona matokeo hayo kwa sababu tumbo bado litakuwa limezungukwa na mafuta. 

Jinsi ya kupunguza mafuta katika mwili; 
Kuna usemi unaosema, kwa matokeo ya mazoezi unahitaji.. “ASILIMIA 70 DAYATI, ASILIMIA 30 ZOEZI!”. Kwa matokeo mazuri na ya haraka njia hii hutoa matokeo mazuri Zaidi tofauti na kupiga mazoezi pekee ambapo ni kweli unaweza kuwa unaunguza mafuta mwilini ila hauwezi kuunguza mafuta yakutosheleza kwa siku kuweza kuonyesha matokeo mazuri ya mazoezi unayopiga. 

Ila kwa njia ambayo itakupa matokeo ya muda mrefu maara nyingi huwa ni ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu, na matokeo haya nayaita ya muda mrefu maana mazoezi hayo yatakufanya uwe na adabu ya kubadilisha mwenendo wa maisha yako na kuutunza mwili wako kwa heshima. 

Njia ya 70 kwa 30 inatoa matokeo mazuri maana asilimia 70 ya upunguaji wa mafuta mwilini hufanywa na dayati ya kuangalia nini cha kula na kipi cha kuondoa kabisa kwenye mlo wako wa kila siku. Hata hivyo kwa kuangalia dayati pekee haiwezi kukupa matokeo mazuri, maana tafiti mbali mbali za kisayansi juu ya kupunguza mafuta mwilini zimeonyesha huwezi kupunguza mafuta mwilini kwa dayati pekee na kupata mwili wa kuvutia pasipo kufanya aina yeyote ya mazoezi ya mwili, ukitaka mwili uliopungua kwa mpangilio na mvuto lazima uhusishe pia mazoezi ya mwili. 

Njia kuu ya kupunguza mafuta kwa njia ya dayati ni kupangilia milo yako ya siku; 
Lazima ujue mlo wako utaupangilia katika hali gani, kwa mfano badala ya kula ovyo hovyo, unatakiwa upangilie milo yako kwa kula kiasi, kama umezoea kujaza tumbo wakati wa kula, jaribu kushusha mlo wako uwe unakula kwa kuondoa njaa kwa kuupa mwili vile virutubisho unavyovihitaji tu, na unaweza kula milo mitatu mpaka mitano kwa siku na usizidishe zaidi ya hapo. 

Hakikisha unakula mlo kamili ila kwa kuhakikisha huli vyakula vilivyotengenezwa kwa sukari, na zingatia kuachana na milo inayotayarishwa kwa haraka, (fast sood) kama chipsi, vitafunwa na vinginevyo vinavyohusiana na hivyo, zingatia kula vyakula vyenye protini na milo yako iwe kamili na hasa pendelea kula mboga mboga.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad