Onyo Watakaochoma Matairi Mwaka Mpya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Jeshi la Polisi nchini limepiga marufuku uchomaji wa matairi ambayo yamekuwa yakiharibu miundombinu mingi kama vile barabara ambazo zimejengwa kwa gharama kubwa pamoja na kuleta kero kwa raia wema.

 

Taarifa ya Kamishna wa Polisi, Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba iliyetolewa kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Polisi imepiga marufuku uchomaji wa matairi  sambamba na Disko toto kote nchini na imelekezwa kuwa watoto washerehekee chini ya uangalizi wa wazazi au walezi.


Jeshi la polisi limewataka wananchi watakao kuwa wamekusanyika katika fukwe za bahari na maziwa  kwa ajili ya kusherehekea sikukuu kurejea majumbani mwao mara ifikapo saa kumi na mbili jioni.


Aidha Jeshi la Polisi limesema limejipanga vizuri kuhakikisha  hali ya ulinzi na usalama inaimarishwa  kwa kiwango kikubwa kwa kuelekeza  makamanda  wa Mikoa  kuimarisha ulinzi kwenye nyumba za ibada na maeneo mengine ambayo wananchi watakusanyika huku likitoa wito kwa kila mtanzania kutii sheria kwa hiari kwani hakuna atakaye vumiliwa endapo atavunja sheria.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad