Polisi Tisa Wahukumiwa kwa Mauaji ya Mchuuzi wa Samaki

 


Mahakama moja nchini Misri imewahukumu kifungo cha miaka mitatu maafisa tisa wa polisi kwa kosa la kumtesa na kupelekea kifo cha mchuuzi mmoja wa samaki. 

Taarifa hiyo imeelezwa na duru za mahakama nchini humo. 


Hukumu hiyo ni hatua isiyo ya kawaida ya maafisa kukabiliwa na mkono wa sheria katika nchi hiyo ambako taasisi za kiusalama aghalabu hutuhumiwa kwa unyanyasaji. 


Maafisa hao wa polisi wanaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo kwa mujibu wa duru. 


Mashirika ya haki za binadamu mara kwa mara yamekuwa yakizishutumu idara za usalama nchini Misri kwa unyanyasaji na utesaji madai ambayo yamekuwa yakipingwa na wizara ya mambo ya ndani nchini humo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments