Prince Harry na Meghan Wamelamba Dili Nono Mtandao wa Spotify


Kama wewe ni miongoni mwa wapenda Podcast basi jiandae kuisikiliza hii ya Prince Harry na mkewe Meghan Markle, wawili hao wamelamba dili nono la kufanya Podcast katika mtandao wa Spotify, dili lenye thamani ya (£30m) sawa Bilioni 92 za Kitanzania.

Dili ya kupata Podcast hiyo ambayo itaanza kuruka baadaye mwezi huu imedaiwa kusukumwa sana na Meghan Markle, ikiwa ni miezi michache tu tangu wajitenge kwenye familia ya Kifalme.

Hii inakuwa dili yao ya pili pamoja, mapema mwezi Septemba mwaka huu iliripotiwa kwamba wamelamba mkataba mnono toka Netflix kwa ajili ya kutengeneza maudhui mbali mbali ikiwemo Documentary, Filamu, Vipindi na Docu-Series, mkataba uliotajwa kuwa na thamani ya ($100m) sawa na takribani TSH. Bilioni 231.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments