Radi yauwa watoto wawili wa familia moja Songwe

Na, Baraka Messa, Mbozi.
RADI yaua watoto wawili wa familia moja na kujeruhi wazazi katika Kijiji Cha Shasya kata ya Halungu Wilayani Mbozi Mkoani Songwe .

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Wizman Mwashibanda alisema tukio hilo limetokea Desemba 15 saa nane mchana.

Alisema baada ya kusikia sauti kubwa ya radi alifika haraka eneo la tukio na kukuta watoto wawili Miznala Mgale (4) na dada yake Edna Mgale wakiwa tayar wamepoteza maisha katika vyumba tofauti huku mama wa watoto hao akiwa akiwa amejeruhiwa na kupoteza fahamu jikoni.

Alisema baada ya tukio Hilo desemba 16 marehem hao wamezikwa , huku mama yao akiendelea na matibabu katika hospital ya Mbozi Mission aliko kimbizwa baada ya tukio Hilo.

Baba wa watoto hao waliopoteza maisha Mawazo Mgale akizungumzia tukio Hilo kwa masikitiko makubwa ,alisema tukio Hilo lilitokea ghafla na radi kupiga vyumba vyote vitatu vya nyumba yake , ambapo yeye alikuwa sebuleni na mtoto wake Miznala (4) aliyefariki hapo hapo, mtoto wake Edna (14) alikuwa kwenye chumba kingine ambapo naye alifariki hapohapo huku mama yao aliyekuwa jikoni akijeruhiwa vibaya.

"Mimi baada ya tukio Hilo me guu yote ilikufa ganzi lakin baada ya muda mwili ulirudi katika hali yake ya kawaida"  alisema Mawazo.

Diwani wa kata hiyo ya Halungu Maarifa Mwashitete alisema tukio hilo limewashitua na kuwa sikitisha Sana , huku akidai kuwa tukio aina hiyo kwa kata hiyo ni Mara yake ya Kwanza kutokea katika kata hiyo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments