Rais Macron wa Ufaransa Akutwa na Corona

RAIS wa Ufaransa,, Emmanuel Macron (42), amekutwa virusi vya corona na ana dalili za wazi hivyo atajitenga kwa siku saba.  Vilevile, Waziri Mkuu, Jean Castex,  atajitenga kwa kuwa ni mtu aliyechangamana na rais huyo.

 

Mapema wiki hii Ufaransa iliondoa zuio la kubaki ndani, maambukizi yalivyoongezeka pakalazimika kuweka ‘curfew’ ambayo ni kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.

 

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, Ufaransa imerekodi maambukizi milioni mbili tangu Corona iingie nchini humo na vimeripotiwa vifo  zaidi ya 59,400.  Jumatano wiki hii paliripotiwa maambukizi mapya 17,700.

 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments