Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rais Mwinyi Ateua Ma DC, Wapo HapaRAIS wa Zanzibar, Hussein Mwinyi, amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya (DC) kumi visiwani humo.

Uteuzi huo ameufanya jana Jumatatu tarehe 28 Desemba 2020 na kutangazwa kwa umma na Hassan Khatib Hassan, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya Hassan, uteuzi wa wakuu hao wa wilaya, ulianza jana Jumatatu.

Walioteuliwa na wilaya zao kwenye mabano ni, Rajab Ali Rajab (Mjini). Kabla ya uteuzi huo, Rajab alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B.

 

Khamis Mbeto Khamis (Magharibi A), Hamida Mussa Khamis (Magharibi B), Aboud Hassan Mwinyi (Kaskazini A), Kassim Haidar Jabir (Kaskazini B), Sadifa Juma Khamisi (Kusini-Unguja) na Marina Joel Thomas (Kati). Kabla ya uteuzi huo, Marina alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini.

 

Wengine ni; Mgeni Khatib Yahya (Wete), Mohammes Mussa Seif (Micheweni). Kabla ya uteuzi huo, Seif alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete na Abdallah Rashid Ali ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake).


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments