Rapper Lil Wayne Rapper Auza nyimbo zake zote (Master Recording) kampuni ya Universal Music Group


Rapper Dwayne Carter #LilWayne, ameripotiwa kuuza haki za nyimbo zake zote (Master Recording) kwa kampuni ya Universal Music Group kwa kiasi cha dola Milioni 100 ambazo sawa na TSh. Bilioni 231.


Kwa mujibu wa TMZ, ambao walifanikiwa kupata nyaraka za Mahakama kuhusiana na hilo, umeeleza kuwa #LilWayne (38) ameuza Master Recording na kuwaachia Universal Music Group, ambayo ni moja ya Label kubwa za muziki duniani kitendo ambacho mashabiki wa muziki wameonekana kukasirishwa nacho.


Pia mastaa wakubwa duniani wameshangazwa na uamuzi huo wa #Wayne ambapo hadi sasa hawajui jamaa huyo alipatwa na nini.


Itakumbukwa, Mwimbaji #TaylorSwift siku za hivi karibuni alithibitisha kuwa haki za albamu zake sita za kwanza zimeuzwa bila ya yeye kujua, hali iliyopelekea kuwepo na mzozo mkubwa hadi kufikishana Mahakani, baina yake na uongozi wake wa zamani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments