Rose Mhando Shavu Dodo
STAA wa muziki wa Gospol Afrika Mashariki, Rose Muhando ameyashinda majaribu ya umauti na sasa ameibuka upya akiwa amenawiri ‘shavu dodo’ na kuwa na nuru usoni.

Rose ambaye kwa sasa kazi zake nyingi anafanyia nchini Kenya, amerejea katika ubora wake ikiwa imepita miezi kadhaa bila kusikika kwa kuachia wimbo mpya.

 

Katika mahojiano na Gazeti la IJUMAA njia ya simu, Rose anasema kuwa amerejea kwenye ubora wake.
Ameeleza kuwa, kutokuonekana kwake katika huduma ya neno la Mungu kwa njia ya nyimbo za Injili.

 

Mwanamama huyo anasema kuwa, amekaa nje ya huduma kwa muda akijifunza mambo mengi, lakini sasa amerejea kwa kishindo kwa ajili ya kutoa huduma kwa watu wa Mungu.

“Ni kweli watu wa Mungu walinikosa kwa muda, lakini waambie nimerejea kwenye kiti changu,” anasema staa huyo wa Wimbo wa Utamu wa Yesu.

 

Rose anasema kuwa, baada ya kurejea upya ameachia wimbo mmoja na mwimbaji maarufu wa Kenya, Size 8 unaoitwa Vice Versa  katika picha zake alizoachia kwenye ukurasa wake wa Instagram wikiendi iliyopita, Rose anaonekana kuwa mrembo na aliyenenepa, tofauti na alivyozoeleka.

Ndiyo, Rose sasa hivi anaonekana ni mwanamke mrembo kwelikweli kiasi cha kumshangaza kila mtu. “Ninamshukuru Mungu ninaendelea vizuri na ninawashukuru wote walionisaidia wakati wa majaribu,” amesema

 

Rose ambaye mara ya mwisho aliachia wimbo uliokwenda kwa jina la Kenya Ulindwe akimshukuru Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na wananchi wake kwa namna walivyompa sapoti alipokuwa akiumwa.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments