Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Seven; Mrembo Shujaa, Daraja la Mastaa Kibao Bongo!

UNAPOZUNGUMZIA wadau wa muziki Bongo, huwezi kuacha kulitaja jina la Christine Mosha au Seven kama vile ambavyo watu wengi zaidi wanamfahamu kwa jina hilo.

 

Seven ambaye nyota yake ilianzia kung’aa kiburudani kuanzia kwenye eneo la utangazaji, amefanya kazi na mastaa wengi wakubwa nchini ambapo ukisema utaje orodha yake huwezi kuimaliza yote.

 

Watu wengi wamemfahamu zaidi Seven kwenye kipindi cha AliKiba, walipokuwa wakifanya kazi pamoja kupitia kampuni ya Rockstar 4000 lakini mbali na Kiba, legendary Judith Wambura ‘Jide’, Omari Nyembo na wengine wengi wanatambua mchango wa mwanadada huyu katika muziki wao kama meneja.

 

Hapa katikati kulipita ukimya kidogo kwa Seven baada ya Kiba kutangaza kuwa hatakuwa naye kwenye eneo la kumsimamia, bali atafanya naye kazi kwenye mlengo mwingine na mkali huyo akamtangaza meneja wake mpya ambaye hata hivyo kwa sasa naye ameshaachana naye.

 

Baada ya ukimya huo kupita, taarifa mpya kutoka kampuni kubwa duniani ya Sony Music zimeeleza kuwa, wamemteua kuongoza Kitengo cha Masoko na Maendeleo ya Wasanii Afrika Mashariki ambapo atainua masoko ya wasanii katika nchi takriban 14.

 

Nchi hizo ni; Tanzania, Kenya, Uganda, Congo DR, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Eritrea, South Sudan, Somalia, Malawi, Zambia na Zimbabwe.

 

Seven akianza kazi rasmi, anatarajiwa kujenga orodha ya kampuni ya vipaji vya eneo hilo na kukuza kazi zake za kimataifa na zilizopo katika eneo hilo kutokea makazi yake nchini Tanzania na ataripoti moja kwa moja kwa Sean Watson, Mkurugenzi Mtendaji, Sony Music Africa.

 

Kwa upande wake Seven, amesema kwake yeye ni furaha kubwa kuifanya kazi hiyo anayoipenda:

“Sony Music ina historia kubwa kwenye tasnia ya muziki duniani, kwa hiyo kuwa sehemu ya kampuni hii katika wakati huu wa kazi yangu inaonekana ni toshelezo zuri ambapo nitaleta uzoefu na utalaamu wangu kibiashara kwenye kampuni nzima.”

 

Seven analeta uzoefu wa miaka 15 katika tasnia ya muziki ya Afrika katika kazi hiyo na amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na Sony Music Africa kwa miaka mingi.

 

Kupitia hilo, Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania pia umempongeza kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo wamesema, wanaamini atakuza ushirikiano kati ya wanamuziki wa Tanzania na Marekani.

Kama hiyo haitoshi, Seven ameandikwa pia kwenye mtandao wa Billboard ambao una heshima kubwa Marekani na duniani kote.

 

Ikumbukwe tu, mwaka 2017 alianzisha lebo yake binafsi ya muziki na kampuni ya kusimamia vipaji, Rockstar Africa ambako alichochea mafanikio kibiashara kwa wasanii wengi wa muziki wa Afrika Mashariki wakiwemo Lady Jaydee, Ray C, TID, Rose Muhando, Xtatic, Alikiba na Ommy Dimpoz.

 

Tangu 2010, Seven ameiongoza pia Rockstar 4000 Music Entertainment, kampuni ya kwanza ya muziki ya Afrika inayojitegemea pamoja na mtandao wa utayarishaji wa maudhui, kidigitali na matukio.

 

Huko, mwanamke huyu shupavu alisimamia uchapishaji wa muziki, mikataba ya muziki na leseni za maudhui akiwa na Sony Music Africa, ikiwemo kufanya kazi kwenye kampeni kwa ajili ya kombe la dunia la FIFA 2010 lililofanyika Afrika Kusini.

 

ALIANZIA WAPI?

Mosha alianza kazi yake mwaka 2006 kama mtangazaji wa redio wa kipindi cha asubuhi, promota na gwiji wa masoko Clouds Media Group kabla ya kuhamia MTV mwaka 2005 ambako aliongoza kitengo cha wasanii na kazi pamoja na biashara barani Afrika.

 

Alizindua kituo cha MTV Base Tanzania, na akifanya kazi kwenye miradi ikiwemo Staying Alive Campaign akiwa na Kelly Rowland nchini Tanzania pamoja na ziara ya Water for Life iliyoshirikisha Umoja wa Mataifa, Clouds Media na Jay Z.

 

Katika miaka mitano iliyofuata hadi alipoanzisha Rockstar Africa, Mosha alikuza orodha ya kazi alizofanya kuwajumuisha wasanii kama Alikiba (Best African Act katika MTV Europe Music Awards mwaka 2016) na Ommy Dimpoz (Best Male East Africa katika tuzo za AFRIMA mwaka 2019), pamoja na watayarishaji wa muziki, wanamichezo na waigizaji.

MAKALA: ERICK EVARIST

 


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments