Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Shamsa, Amwomba Radhi Chidi Mapenzi Madongo Aliyomrushia
MSANII wa Bongo Movie, Shamsa Ford, amevunja ukimya na kuamua kusamehe yale yote aliyokosana na aliyekuwa mume wake, Chidi Mapenzi, huku akisema hatasahau imani na wema aliotendewa na mwanamume huyo.

 

Shamsa, kwa kupitia mitandao wa kijamii, amesema; “Tulipoachana tulikuwa maadui wakubwa lakini namshukuru Mungu akaweka wepesi juu yetu. Mimi na wewe tunajua hatuwezi kurudiana na haitotokea tena sababu kila mtu ameendelea na maisha yake, hunipendi kimapenzi na mimi sikupendi kimapenzi tumebaki ndugu wa kusaidiana.

 

“Siku nilipokusamehe Mungu alinifungulia baraka nyingi mpaka nikashangaa. Kumbe sikujua nilikuwa najifunga nilipobeba vitu moyoni. Rashid nimeongea mengi mabaya kuhusu wewe, yote ni kwa sababu ya hasira na kidonda kilikuwa kibichi. Pamoja na yote uliyonikosea lakini siwezi kusahau wema wako.

 

“Rashid asante sana kwa kunipa nafasi kipindi nilipokuwa mkeo kukaa dukani kwako maana si kila mwanamume anaweza akamruhusu mkewe akae sehemu yake ya kazi.  Umenifunza biashara na nikakomaa kwenye biashara mpaka leo hii naishi, nasomesha, nalea familia kwa ajili ya hii biashara.

 

“Rashid pamoja na mabaya yote haimaanishi kwamba hukuwa na jema kwangu. Rashid asante sana kwa huruma yako juu yangu 😭😭 dah unajua namaanisha nini. Namshukuru Mungu sina kinyongo na wewe tunaweza tukasalimiana tukikutana hata nife kesho najua utanizika na mimi nitakuzika.

 

“Mungu akutangulie inshaallah kwenye biashara yako izidi kukua najua wewe ni mpambanaji na uhakika utafikia malengo yako. Mungu akusaidie upate mke mwema zaidi nilivyokuwa mimi akutunze inshaallah nitafurahi sana…. “

 L

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments