Shamsa Ford Amshushia Ujumbe Mzito Chiddi Mapenzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Muigizaji na mfanyabiashara Shamsa Ford amemuandikia ujumbe mzito aliyekuwa mume wake Chidi Mapenzi kwa kumwambia amemsamehe, hana kinyongo naye na hata mmoja wapo akifariki watazikana.

Katika ujumbe huo alioandika Shamsa Ford kupitia ukurasa wake wa Instagram unaeleza kuwa  "Tulipoachana tulikuwa maadui wakubwa lakini namshukuru Mungu akaweka wepesi juu yetu, mimi na wewe hatuwezi kurudiana na haitotokea tena, kila mtu ameendelea na maisha yake tumebaki ndugu wa kusaidiana" 

"Siku nilipokusamehe Mungu alinifungulia baraka nyingi mpaka nikashangaa kumbe sikujua nilikuwa najifunga nilipobeba vitu moyoni, nimeongea mengi mabaya kuhusu wewe yote ni kwa sababu ya hasira na kidonda kilikuwa kibichi" 

"Namshukuru Mungu sina kinyongo na wewe tunaweza tukasalimiana tukikutana hata nife kesho najua utanizika na mimi nitakuzika, Mungu akusaidie upate mke mwema zaidi nilivyokuwa mimi akutunze inshaallah nitafurahi sana" ameongeza 

Shamsa Ford ameshusha ujumbe huo baada ya kuwa-post na kuwashukuru watu wake wa karibu ambao wamemtendea wema na wale walioacha alama kwenye maisha yake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad