Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simba Hasira Zote Kwa Majimaji Leo Kwa Mkapa
VITA kubwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar leo Jumapili ni kati ya mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports maarufu FA, Simba ambao wataunguruma dhidi ya Majimaji kwenye mchezo wa hatua ya raundi ya tatu.

 

Mchezo huu utapigwa majira ya saa 1:00 usiku ambapo Simba itaingia uwanjani ikiwa na hasira za kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya FC Platinum mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumatano iliyopita.

 

Inakutana na Majimaji ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ikiwa Kundi A na mchezo wake uliopita ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Boma FC.Mshindi wa mchezo wa leo anatinga hatua ya nne hivyo ni vita ya kutetea ubingwa dhidi ya ile ya kuvua ubingwa ambayo ni nia ya Majimaji FC.

 

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck ameliambia Spoti Xtra kuwa wanahitaji Kombe la Shirikisho hivyo njia pekee ni kupata ushindi kwenye kila mechi.“Tuna malengo ikiwa ni pamoja na kutwaa Kombe la Shirikisho, hivyo hatuna chaguo, wapinzani wetu tunawaheshimu ila tunahitaji matokeo bora,” alisema Sven.

 

Meneja wa Majimaji, Godfrey Mvula, ameliambia Spoti Xtra kuwa wamejipanga kuifunga Simba licha ya kwamba inashiriki mashindano ya kimataifa.Mbali na mchezo huo, pia kutakuwa na mchezo kati ya Namungo dhidi ya Green Warriors, Uwanja wa Azam Complex, Dar na Mtibwa Sugar v Geita Gold Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

 

Yanga wao hawana presha washatinga hatua ya nne baada ya wapinzani wao Singida United iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza kushushwa madaraja mawili.

Stori na LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments