Simba Waikazia Yanga Dar, Kuingia Uwanjani Lazima Uvae Jezi ya Simba

 


KATIKA kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United ya Nigeria, uongozi wa Simba umetangaza kuwa mashabiki 30,000 ndiyo wameruhusiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuingia uwanjani kushuhudia mchezo huo.


Katika suala hilo, Simba wameonekana kuwakazia Yanga kwa kusema kwamba siku hiyo mashabiki hao 30,000 wanataka wote wawe wamevaa jezi za Simba


Katika mchezo uliopita ambao Simba walikuwa ugenini kwenye Uwanja wa New Jos, Nigeria, walifanikiwa kuibuka na ushindi bao 1-0.

Ofisa Habari wa Simba, Manara alisema: “Tunafahamu kuna mashabiki wanaojiandaa kuja uwanjani kwa ajili ya kutuzomea bila ya kufahamu hilo ni tukio la kitaifa, hivyo basi niwaombe wabakie nyumbani kwao.

“Hatutawaruhusu mashabiki wa aina nyingine tofauti na Simba kuingia uwanjani, tunataka mashabiki

30,000 tulioruhusiwa na CAF kuingia uwanjani wote wawe wa Simba.

Kwa upande wa Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda, alisema: “Tumedhamiria kufanya makubwa msimu

huu katika michuano hii mikubwa Afrika, kikubwa ni kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, tunafahamu tuna kibarua kigumu kwa Plateua katika mchezo wa marudiano.”

Viingilio vya mchezo huo vitakuwa hivi; Platnum Sh 150,000, VIP A Sh 40,000, VIP B na C Sh 20,000, huku mzunguko ikiwa ni Sh 7000. Tiketi zilianzwa kuuzwa jana Jumatano.

Stori Na WILBERT MOLANDI NA

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments