Simba Wanaiwaza FC Platinum Desemba 23
KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameweka wazi kwamba kwa sasa akili zake zipo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.

 

Simba imetinga hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwaondoa Plateau United ya Nigeria kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0. Desemba 23, mwaka huu, inatarajia kukutana na Platinum ya Zimbabwe.Marudiano ni Januari 6, mwakani.Akizungumza na Spoti Xtra, Sven alisema: “Nadhani ipo wazi kwamba tuna kazi kubwa kimataifa, nikiwa kwenye mchezo wa ligi nina kazi ya kufikiria pia namna nitakavyoweza kupata matokeo kwenye mchezo dhidi ya FC Platinum.“

 

Ukicheza ugenini hasa kwenye mechi kama hizi nafasi za kufunga mabao zinakuwa chache, hivyo tuna jukumu la kutumia hata ile moja ambayo tutaipata.“Lakini pia licha ya kutumia nafasi tunatakiwa kuwa bora zaidi kwenye eneo la ulinzi kwa kutofanya makosa ambayo yatatugharimu kwa namna yoyote ile.”Naye kipa namba moja wa kikosi hicho, Aishi Manula, alisema: “Tunaitumia mechi yetu ya KMC kama sehemu ya kujiandaa na mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Platinum, tunatumia mchezo huu kutupa taswira kuelekea mechi yetu ya kimataifa ili tuweze kufanya vizuri.“

 

Pia tuna malengo makubwa ya kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo, tuna kila sababu ya kutafuta pointi tatu kwa udi na uvumba na ukiangalia tupo nyuma katika msimamo wa ligi, hivyo tunahitaji kupambana ili tuweze kuwa kileleni kama tulivyozoea na kutwaa ubingwa wa ligi.”Jana Jumatano, Simba ilipambana na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

WAANDISHI: LUNYAMADZO MLYUKA, SAID ALLY NA KHADIJA MNGWAI

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments