Simba Warudi na Kiungo wa FC Platinum

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




JINA la kiungo mshambuliaji wa FC Platinum, Perfect Chikwende limeingia kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na timu hiyo katika usajili huu wa dirisha dogo uliofunguliwa Desemba 16, mwaka huu.

Simba tayari imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Mganda Taddeo Lwanga katika dirisha dogo huku ikiwa kwenye mipango ya kusajili mshambuliaji na beki mmoja wa kati atakayesaidia kucheza na Pascal Wawa, Joash Onyango na Erasto Nyoni.

 

Chikwende ndiye alikuwa mfungaji wa bao la Platinum ilipocheza dhidi ya Simba katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa nchini Zimbabwe.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, Simba imemuweka kwenye rada kiungo huyo msumbufu mwenye uwezo wa kuzuia na kushambulia kwa nguvu wakati akiwa na mpira.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa Simba ilianza kuvutiwa na kiungo huyo mara baada ya kucheza na Platinum na kuonyesha kiwango kikubwa kilichowavutia mabosi hao waliokuwemo katika msafara uliokwenda Zimbabwe.

 

Aliongeza kuwa timu hiyo inataka kumsajili kiungo huyo kutokana na tetesi za Mzambia, Clatous Chama kuihama timu hiyo mwishoni mwa msimu huu kwenda kucheza nje ya nchi.“Tetesi zipo kuwa Chama anaweza akatimka Simba mwishoni mwa msimu huu kipindi ambacho mkataba wake unamalizika, hivyo wamepanga kumsajili Chikwende kwa ajili ya kuchukua nafasi yake.“

 

Hiyo ni baada ya kuvutiwa na kiwango ambacho amekionyesha katika mchezo wa kwanza tuliocheza Zimbabwe, kwani ndiye mchezaji aliyekuwa msumbufu kwa mabeki wetu tofauti na bao alilolifunga.“Uzuri ni kwamba kocha mwenyewe Sven (Vandenbroeck) ameuona uwezo wake, hivyo kama mipango ikienda vizuri basi upo uwezekano wa kumalizana na kiungo huyo katika dirisha dogo la msimu huu,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ hivi karibuni alisema kuwa: “Tumepanga kuziboresha baadhi ya sehemu kwa kupitia ripoti ya kocha, wapo wachezaji tulio kwenye mazungumzo nao na baada ya taratibu kukamilika za usajili, basi tutawaweka wazi.“

 

Tupo tayari kusajili mchezaji yeyote tutakayemhitaji katika dirisha dogo kwa gharama zozote, kikubwa ahitajike na kocha kwani yeye ndiye tumempa jukumu hilo lote la usajili.”Katika hatua nyingine, Azam FC nayo inatajwa kuwemo kwenye rada za kuwania saini za kiungo huyo katika usajili huu wa dirisha dogo katika kuimarisha safu ya kiungo.

 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad