Stamina Ameweka Wazi Kupata Mtoto wa Kiume..Ampa Jina la Mchezaji Huyu


Rapa Stamina @staminashorwebwenzi kutoka kundi la ROSTAM, ameweka wazi kupata mtoto wa kiume hivi karibuni aliyempa jina "Lionel" na mwishoni mwa wikiendi iliyoisha ametimiza 40.


#Stamina ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania,  ameshare picha ya kijana wake huyo wa kiume kupitia ukurasa wake wa instagram, aliyempa jina la mchezaji wa timu ya Taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi.


Akieleza juu ya jina Lionel ambalo amempa mwanae, #Stamina amesema, kwa mapenzi aliyonayo kwenye soka, na mchezaji wake bora ni #Messi, hivyo akampa jina la mchezaji huyo mwanae.


"Ndoto za watu wengi duniani hapa ni kupata mtoto/watoto kama tulivyoagizwa katika vitabu vitakatifu, kuwa tukazaliane na kuijaza dunia!! Asante Mungu kwa kuniletea kiumbe huyu mpya duniani, and now I’m officially a father.


"Ungekuwa wa kike ningekupa jina la mama yangu ili kumuenzi huko kaburini. Lakini kwakuwa ni wa kiume na kwa mapenzi niliyonayo kwenye soka, na mchezaji wangu bora ni #Messi nimekupa jina nawe utaitwa #Lionel.


"Mungu akujalie afya njema na ridhiki ya kutosha, akulinde milele yote,uishi kwenye maadili ya kumpendeza yeye siku zote!! Dunia ina mambo mengi mwanangu, Kua salama Ukayashuhudie!! umetimiza 40 jana🙏" ameandika Stamina.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments