Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Steve Harvey "Niliitwa Nikachekeshe Bure Sikuwa Hata na Nauli Nilikopa, Lakini Baada ya Kuchekesha Pale Dunia ilinilipa"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Steve Harvey alialikwa kwenye tamasha moja huko Las Vegas kwenda kuchekesha lakini ilikuwa bure hakulipwa kitu chochote. Ukiacha kutolipwa tu hata nauli ya kwenda Vegas alikopa hakuwa na pesa mfukoni. Alipewa dakika 15 za kuzungumza ambazo zitawafanya watu wacheke.

Anasema alipomaliza dakika15 za mwanzo aliongezwa nyingine kwasababu watu walikuwa wamefurahi sana na zile dakika15 za mwanzo. Anasema tokea hapo ndio ulipofunguka mlango wa mafanikio yake na kuwa mtu maarufu na mwenye kipato cha juu kwasababu ya uchekeshaji. Kumbuka kuwa alichekesha bure na hata pesa ya kumfikisha kwenye tamasha alikopa.

Lakini baada ya tamasha Steve hakuwa yule aliekuwa kabla ya tamasha. Unatakiwa kufahamu kuwa hakuna kitu cha bure katika hii dunia. Chochote unachofanya hata kama hautolipwa kitu mkononi basi utalipwa kwa thamani yako kuongezeka. Kama Steve angeweka kulipwa mbele asingekuwa hapo alipo leo.

Onesha ulichonacho kwanza ndio dunia ikulipe usitake malipo kabla hujaonesha ulichonacho. Dunia ipo macho na inakuangaza kuliko udhaniavyo ukiinua tu hatua basi itakulipa kwa gharama uitakayo. Hakuna kitu cha bure hata kama wewe unahisi unafanya bure ila ipo siku bure yako itakupa thamani na dunia itakulipa.

Post a Comment

0 Comments