Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tabwe Afunguka "Yanga Wanapaswa Kulipa Fedha Zote, Wasipofanya Hivyo Watajuana na Fifa"

 


NYOTA wa zamani wa Yanga, Amiss Tambwe amesema kuwa ikiwa timu hiyo haitamlipa fedha zake za usajili pamoja na mshahara wake watajuana na Shirikisho la mpira duniani, (Fifa) kwa kuwa yeye hausiki kwenye kutoa hukumu. Tambwe amesema kuwa ameambiwa na mwanasheria wake kwamba kesi yake dhidi ya Yanga ameshinda hivyo kinachotakiwa ni Yanga kumlipa fedha zake anazodai.
"Mwanasheria wangu ameniambia kwamba tumeshinda kesi hivyo kinachotakiwa ni Yanga kulipa hizo fedha kama hawatalipa ni wao watajuana na Fifa mimi sijui itakuaje.
"Tulichokifanya tumewapa akaunti namba Yanga kisha tunasubiri  kuona fedha zinaingizwa. Tena zinapaswa kuingizwa zote kwa kuwa ingekuwa kidogokidogo ni wakati ule tungekubaliana ila kwa sasa hilo halipo," .


Mahakama ya Usuluhishi masuala ya michezo (CAS) imeamuru Yanga kumlipa Amisi Tambwe dola 20,000 (46.4 M Tsh) pesa ambazo alikuwa anaidai klabu hiyo kama ada ya usajili na mshahara wa miezi mitatu.


Mshambuliaji huyo aliachwa na Yanga msimu wa 2018/19 kwa kile kilichoelezwa kuwa amechukua ubora wake.
Tambwe aliondoka Yanga akiwa na madeni yake hayo ambayo klabu hiyo haikumlipa kwa wakati kiasi cha kuwashitaki CAS na chombo hicho kutoa hukumu alipwe ndani ya siku 45 kuanzia Desemba 1, 2020. 


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments