Takukuru Yarejesha Mil 5.48 za Mwalimu Aliyetapeliwa na Qnet
TAASISI  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita imemrejeshea Rose Mgomba, mwalimu wa Shule ya Msingi Lukaranga, Sh. milioni  5.48 ambazo alidhulumiwa na kampuni ya QNET kwa kumrubuni kwa ahadi za uwongo.

 

Mwalimu huyo aliahidiwa kutengeneza faida ya fedha maradufu baada ya kuwezeshwa kufungua akaunti ya ununuzi wa bidhaa za kampuni hiyo mtandaoni.

 

Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, Leonidas Felix,  amewataka wananchi na watumishi wa umma,  hasa walimu, wajiepushe kujiunga na biashara wasizokuwa na uhakika nazo.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments