Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tanasha: Mondi Ameanza Kutoa MatunzoMZAZI mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna amesema kuwa, jamaa huyo sasa ameanza kutoa pesa ya matunzo ya mtoto wao, Naseeb Junior.

 

 

Awali, mara tu baada ya kutengana na Diamond au Mondi, mapema mwaka huu, Tanasha alilalamika kuzidiwa na majukumu ya kumlea mtoto wao huyo peke yake.

 

 

Tanasha anasema kuwa, kwa sasa anapumua kwa sababu Mondi anamuhudumia mtoto wao huyo, jambo ambalo anajivunia mno.

 

Ikumbukwe kwamba, wawili hao waliachana baada ya kujaaliwa mtoto huyo wa kiume na kufanya muziki pamoja, wakitingisha na wimbo wao wa Gere.

 

Akizungumza akiwa nyumbani kwao nchini Kenya, Tanasha anasema kuwa, kwa sasa anaona jitihada za Mondi katika kumuhudumia mtoto wao huyo tofauti na hapo awali.

 

“Kwa mwanaye kwa sasa analipa ada ya shule, anafanya vizuri, anafanya jitihada, “Ninaona kile anachofanya kwa mtoto wake, napenda sana jinsi anavyofanya jitihada za kuwa baba mzuri, ninajivunia,” anasema Tanasha ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye muziki.

 

Katika hatua nyingine, Tanasha anasema kuwa nyumba aliyonunua hivi karibuni hakupewa pesa na Mondi kama baadhi ya watu wanavyodai, bali ni katika mambo yake mengine.

 

Hata hivyo, habari za ndani zinasema kuwa, kuna uwezekano wa Mondi kuwachukua wanaye wote kutoka kwa mama zao mara tu baada ya kufikisha umri wa miaka sababu kwa mujibu wa sheria.

STORI: KHADIJA BAKARI, DAR


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments