Tanasha: Simpeleki Mtoto Ng’o
MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Kenya, Tanasha Donna Oketch ambaye pia ni mzazi mwenza wa kinara wa
Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ amewajia juu mashabiki ambao wanataka ampeleke mtoto kwa baba yake na kusema; “Simpeleki huko Madale ng’o!”.

 

Ishu hiyo ilizuka wikiendi iliyopita baada ya mwanamama mjasiriamali kutoka nchini Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutinga Bongo na watoto, Tiffah Dangote na Prince Nillan kwa ajili ya kumsalimia baba yao, Diamond au Mondi.

 

Kama tunavyofahamu watu wa kwenye mitandao hawakosi kuwa na chokochoko, baada ya Zari kurejea Afrika Kusini anakoishi na watoto hao, huku nyuma baadhi ya watu wakaanza kumchokonoa Tanasha ambaye naye amezaa na Mondi mtoto mmoja wa kiume aitwaye Naseeb Junior.

 

Baadhi ya watu wamekuwa wakimuuliza ni lini na yeye atampeleka mtoto kwa baba yake kama alivyofanya Zari na kulala hukohuko ambapo Tanasha yeye amecharuka ile mbaya. “Hivi Tanasha naye anamleta lini mwanaye na yeye tuone kama atakwenda kupokelewa kama alivyofanyiwa Zari? Maana naona kama Zari amewafunika siyo kwa
kupokelewa kule.

 

“Kwanza Tanasha si alishawahi kusema kwamba kumlea mtoto mwenyewe siyo kazi rahisi? Kwa nini na yeye asimlete mtoto kwa baba yake ambaye ana pesa? Ningekuwa ni mimi wala nisingejichosha, mwenzake (Zari) ameshakuja kuchuna za kwake, amesepa,” aliandika mmoja wa mashabiki wa Tanasha.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments