Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tunahitaji Nandy Wengine Kama 10 ili Tushinde


Bongo Fleva haihitaji propaganda kama za Manara ndani ya Simba ili ishinde ama kuongelewa sana. Bongo Fleva hii inahitaji kina @officialnandy wengine 10 ili TUSHINDE.


Uhitaji huo si wa kufanana sauti wala sura, sababu ikiwa hivyo hapatakuwa na jipya zaidi ya kuwa na Nandy 10 kwenye sura moja. Upo uhitaji wa wachezaji 10 wa kike kwenye Game ili Mfumo wa 4-4-2 (Four Four Two) ukamilike, yaani nyuma wanne, katikati wanne na mbele wawili.


Idadi hiyo ya watu 10 ambao ni wasichana kwenye Bongo Fleva itatufanya tuwe vizuri kwenye maeneo kadhaa ikiwemo kuwa vizuri uwanja wa nyumbani na ugenini. Nyumbani tutapata faida ya muziki mzuri ikiwemo video nzuri, ushindani, shows za kutosha pamoja na madili ya Ubalozi ya kutosha.


Ugenini tutafanya vizuri kwenye uwakilishi mzuri wa TUZO kubwa duniani ili tuliwakilishe Taifa vizuri huko kwa wenzetu. Suala la kikosi hicho wao kufaidika tutawaachia ujuzi binafsi, Ila sisi tutafaidika moja kwa moja na muziki mzuri.


Tafadhali wadada, Bongo Fleva bado ipo na washambuliaji wawili wakike kule mbele. Bado media na mashabiki wanahitaji kufanya usajili ili mfumo huo ukamilike, lakini pia Ili tupate kikosi kipana ambacho kitakuwa tayari muda wowote kupambana.

  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

1 Comments

  1. Mimi ndiye nimeiandika hii.Contact nami kwa mazungumzo.0623158177

    ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)