Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

UN yalaani kifungo cha mwanahabari wa China kuhusu corona


Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binaadamu imeleezea wasiwasi kuhusu adhabu iliyotolewa leo na mahakama ya China ya kifungo cha miaka minne jela dhidi ya mwanahabari wa Kichina Zhang Zhan ambaye aliripoti kutokea Wuhan mwanzoni mwa janga la corona. 
Zhan ambaye ni wakili wa zamani, amehukumiwa katika mahakama ya Shanghai kwa madai ya "kuchochea ugomvi" wakati akiripoti matukio ya mwanzo ya mripuko wa corona. Ofisi hiyo imesisitiza mwito wake wa kutaka aachiliwe huru. 

Ripoti zake za moja kwa moja na makala zilisambazwa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii Februari, na kuwafikia maafisa nchini humo ambao mpaka sasa wamewaadhibu watu wanane waliofichua habari za kirusi hicho. 

Umoja wa Mataifa umesema uliilalamikia serikali ya China katika mwaka huu wote wa 2020 ukisema kesi hiyo ni mfano kwa ukandamizaji wa kupindukia dhidi ya uhuru wa kujieleza unaohusiana na COVID-19.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments