Unaambiwa Kung’olewa kwa Spika wa Bunge DRC “Imekuwa Vita Kubwa”

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

  


Muungano wa vyama vya kisiasa wa FCC wa aliyekuwa rais wa DRC Joseph Kabila umekiri kuwa kung’olewa kwa, Jeanine Mabunda kwenye wadhifa wa Spika wa Bunge la nchi hiyo ni vita kubwa na kwamba ulipoteza nafasi muhimu.


Muungano wa FCC ulioanzishwa na Kabila umetoa wito kwa wafuasi wa muungano huo kufunga vibwebwe, wakati wengi wanaendelea kujiuliza maswali kadhaa kuhusu hatma ya FCC.


Baada ya Spika Jeanine kutimuliwa mamlakani na kuvunjwa kwa ofisi ya Bunge (kuondolewa kwa wajumbe 5 kati ya 6 wa kamati kuu ya Bunge), PPRD, chama cha Kabila, hatimaye kimekiri kushindwa.


“Ushindi hauji kila wakati. Wacha tu tufikirie haraka jinsi ya kuimarisha muungano wetu. Maumivu ni makubwa, lakini tusikate tamaa. Wacha tuendelee na vita hivi, wanaharakati wapendwa,” Chama cha PPRD 


Patrick Nkanga, mmoja wa makada wa PPRD, amebainisha kuwa wakati umewadia wa kufanya mabadiliko makubwa kwa Chama cha PPRD na pia kwa Muungano wa FCC. Hii sio mara ya kwanza tunakumbwa na hali hii, huku wafuasi wengine kadhaa wa FCC wakimuunga mkono.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad