Unaambiwa Serikali ya Tanzania Kununua Ndege Zingine Nne

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kuwa serikali iko kwenye mpango wa kunua Ndege zingine 4 ambapo mbili ni za masafa marefu na mbili ni za masafa ya kati, ambazo zitawarahisishia wafanyabiashara wa bidhaa zinazoharibika haraka kusafirisha bidhaa zao kwa uharaka.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 5, 2020, wakati wa uzinduzi wa kongamano la uwekezaji na biashara ya mazao ya bustani, na kuongeza kuwa bidhaa kama minofu ya samaki, mazao ya bustani na nyama yanahitaji kuwa na uhakika wa usafiri.

"Pamoja na Ndege ya mizigo, serikali itanunua Ndege kubwa 2 za masafa marefu na 2 za masafa ya kati ili kuongeza fursa za kibiashara zaidi, pia imeshaunda kamati maalum kwa ajili ya kuainisha changamoto za usafirishaji na kimfumo katika bandari na viwanja vya ndege ili kufanya maboresha yanayohitajika", amesema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu ameongeza kuwa, "Serikali inatambua uwepo wa changamoto katika usafirishaji wa bidhaa, kupitia ilani ya CCM imeweka bayana mpango wa kuboresha mazingira ya usafirishaji wa bidhaa zinazoharibika kwa haraka kwa kunuanua ndege ya mizigo kwa kuzingatia mahitaji ya biashara na ukuaji wa uchumi nchini".


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad