Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Urusi Yaanika Kombora Jipya; ‘Halionekani, Halizuiliki’

RAIS Vladimir Putin wa Urusi amesema nchi hiyo inamiliki kombora ambalo haliwezi kutunguliwa na linaweza kufika pahala popote duniani huku akilielezea kombora hilo kwamba “halipai juu sana, ni vigumu sana kulitambua likipita, lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na linaweza kufika pahala popote pale duniani”.

 

Putin amesema, njia linayofuata haiwezi kutabirika na adui, linaweza kukwepa vizuizi na haliwezi kuzuiwa na mifumo ya sasa ya kinga dhidi ya makombora na hata mifumo inayotarajiwa kuundwa siku zijazo.

 

Kiongozi huyo alisema huku akitumia skrini kubwa, kuonyesha video za kombora hilo jipya.

 

Aidha, amesema kombora hilo haliwezi kuzuiwa na mfumo wa kinga wa makombora wa Marekani Barani Ulaya na Asia na kuonyesha tena video nyingine ya ndege isiyo na rubani inayoweza kufanya kazi chini ya bahari.

 

Kwenye hotuba hiyo yake katika kikao cha pamoja cha mabunge mawili, aliwahamasisha raia kupendekeza majina ya kupewa mifumo hiyo miwili ya silaha.Ulinzi

Putin alisema uwezo wa kijeshi wa Urusi umepangwa na kustawishwa kwa lengo la kudumisha amani duniani. Hata hivyo, amesema iwapo mtu yeyote yule atathubutu kurusha silaha za nyuklia dhidi ya Urusi, atajibiwa mara moja.

 

Alizungumzia pia oparesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Syria, ambapo anamsaidia Rais wa Syria Bashar al-Assad dhidi ya waasi na amesema hiyo inadhihirisha kuimarika kwa uwezo wa Urusi katika kujilinda. 

Urusi ililiteka eneo la Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014 wakati wa uongozi wa Putin ambapo kiongozi huyo amesema Urusi inalinda maslahi yake katika eneo la Arctic kwa kuimarisha miundombinu yake ya kijeshi eneo hilo.

 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments