Waah ya Mondi Yamuibua Mtoto wa Koffi Olomide
BINTI wa Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za Soukous, Antoine Christophe Agbepa Mumba maarufu kama Kofi Olomide, Didi Stone Olomide ameanza kuwadondosha mate wanaume hapa nchini kutokana na urembo wake ambao umewalazimu baadhi ya Watanzania kumwomba aje kuitembelea Tanzania.

 

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni wiki chache zimepita tangu Baba yake atue nchini na kushirikishwa na Msanii wa Bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ katika ngoma iliyokwenda kwa jina la WAAH.

 

Ngoma hiyo ambayo imeachiwa wiki mbili zilizopita, imevunja rekodi katika mitandao mbalimbali ikiwamo Youtube ambako hadi kufikia juzi ilikuwa imefikisha watazamaji milioni 15.

 

Wakati ngoma hiyo ikizidi kushika kasi kama moto wa kifuu, Binti wa mkongwe asiyechuja Koffi Olomide, Didi Stone Olomide naye amesafiria nyota ya baba yake baada ya Watanzania kuanza kummendea.

 

Katika baadhi ya picha alizotumia mrembo huyo ambaye ni mwanamitindo katika jiji la Paris nchini Ufaransa, zimedhihirika kuwakonga Watanzania walioishia kumwomba kuja nchini.

 

“Umefika wakati sasa na wewe uje kuchota nyota ya kutrend hapa Bongo. Karibu sana Tz,” alisema mmoja wa wachangiaji katika akaunti yake ya Instagram.

 

Wachangiaji wengine waliunga mkono na kusema; “Si nguo, si viatu, si nywele zake si kucha, si midomo yake iliyopendeza yaani kila kitu. Hakika huyu ni mwanamitindo anayefahamu vyema kazi yake.

 

“Baba yake huenda kamfu ndisha jinsi ya kuifanya kazi hii ama huenda yeye ndiye humcha gulia mzazi wake mavazi ya ajabu na ya kupendeza ambayo huvalia wakati akipiga muziki wake kwenye steji ama wakati anarekodi video,” aliongeza mchangiaji mwingine.

 

Hata hivyo, mrembo huyo anayedaiwa kuwa hupenda kuzuru nchi mbalimbali na picha zake zinazomuonyesha kuwa mwanamke mwenye figa maridadi.

 

Didi vile vile anaonekana anapenda vipodozi na yuko na mtindo wa kipekee wa kimavazi ambao unatamaniwa na wanawake hasa wa rika lake.

 

Mrembo huyo ambaye kwa sasa amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na urembo wake ni mmoja wa watoto saba wa Koffi Olomide.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments