Wafungwa waliotoroka na kupora shortgun wahukumiwa miaka 30 jela


Mahakama ya Wilaya ya Iringa katika Kesi Na. 139/2020 imewatia hatiani washtakiwa watatu Richard Mbundamila, Taford Kalinga na Haruni Boniface Mgawo na kuwahukumu kifungo cha miaka thelathini (30) jela kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, kutoroka chini ya Ulinzi na Kujeruhi.


Watuhumiwa hao wamehukumiwa kifungo cha miaka thelathini (30) jela kwa kosa la kwanza ambalo ni unyang’anyi wa kutumia silaha na miaka Saba kwa kila kosa kwa makosa ya kujeruhi na kutoroka chini ya ulinzi.


Katika kosa hilo upande wa Mashtaka uliwasilisha vidhibiti kadhaa vikiwemo bunduki aina ya shortgun, mashoka saba, mapanga matano, risasi mbili, maganda mawili ya risasi pamoja nasare za wafungwa tatu.


Ilielezwa Mahakamani hapo kuwa watuhumiwa walikuwa wafungwa waliokuwa wakitumikia vifungo mbalimbali ambapo siku ya tukio walienda kutafuta kuni na wakiwa huko walimvamia askari aliyekuwa anawalinda na kumkata panga kichwani kisha kumnyang’anya bunduki na kuondoka nayo.


Katika tukio hilo mtuhumiwa mmoja aliuawa katika mapambano akiwa huko Njombe ambapo silaha iliyoibiwa ilikombolewa.


Kesi hiyo iliendeshwa na Mawakili wa Serikali Edna Mwangulumba na Brandina Manyanda.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments