Wakazi Amshukia Babu TALE "Usiwasingizie Wafanyakazi wa Taasisi Kwamba Ndio Chanzo Cha Mapishano Yenu"


Ndugu @babutale kama umeamua kufunguka kuhusu machafu yanayotokea nyuma ya pazia kwenye tasnia, BASI FUNGUKA... Ila usiwasingizie wafanyakazi wa Taasisi kwamba ndio chanzo cha mapishano yenu, alafu unataka usihojiwe zaidi na ku-elaborate kwa kisingizio cha "mi muislamu".


Tasnia yetu ina mapungufu mengi, na kuna baadhi ya mapungufu hayo wewe mwenyewe ni chanzo chake. So usitake kutafuta huruma kwa watu na pia kukwepesha ukweli na uhalisia wa yaliyopita.


Tunajua mengi tu, ila tuna vifua vya kuweka akiba ya maneno, ila kama muda umefika wa kuiponya sanaa na tasnia ya Burudani, basi ijulikane na tuache unafiki wa kunyoosheana vidole. #TheLeader

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments