Watu 14 wafariki ajalini Singida

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Watu 14 wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa katika ajali  ya barabarani iliyohusisha basi dogo aina ya hiace na lori katika eneo la Mkiwa wilayani Manyoni mkoani Singida.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Singida, -Sweetbert Chawike amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo usiku wa kuamkia hii leo na kuongeza kuwa basi hilo dogo lilikuwa likitokea mkoani Mwanza likielekea Itigi mkoani Singida na lilikuwa limebeba abiria waliokuwa wakielekea kwenye sherehe za harusi.

Kamanda Chawike amesema lori lililogongana na basi hilo dogo lilikuwa likitoka jijini Dar es salaam na lilikuwa likielekea Kahama mkoani Shinyanga.

Amesema uchunguzi wa awali onaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa hiace ambaye alitaka kulipita gari jingine pasipo kuchukua tahadhari.

Majeruhi watatu wa ajali hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Singida na miili ya watu wote waliofariki dunia katika ajali hiyo imehifadhiwa katika hospitali hiyo.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad