Waziri Jafo Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Geita Mji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mji wa Geita Bw. Modest  Joseph  Apolinary kupisha uchunguzi  kufuatia ununuzi wa gari yenye dhamani shilingi millioni 400 

Akiongea leo na Menejimenti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI Jijini Dodoma Waziri Jafo amesema  kuwa mara baada ya Bunge la 11 la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baraza la Madiwani kuvunjwa majukumu yote yalikasimishwa kwa wakurugenzi na kupelekea baadhi ya  Halmashauri kutumia muanya huo kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.


 “Halmashauri ya Mji wa Geita katika kipindi hicho ambacho baraza la madiwani halipo waliweza kununua gari lenye dhamani ya shilingi milioni 400, jambo hili halikubaliki kwa kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma”amesisitiza Waziri Jafo 


Ameendelea kufafanua kuwa Geita wanafursa nyingi ya madini  lakini  wamenunua gari moja kwa gharama hiyo wakati katika eneo hilo kunauhitaji mkubwa wa vituo vya afya, madawati na vyumba vya madarasa, jambo hili ni kinyume na maadili ya kiutumishi na linarudisha nyuma juhudi za Serikali za kutoa huduma bora kwa wananchi


Waziri Jafo amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga kuunda timu  ya uchunguzi  ambayo itachunguza kwa kina  matumizi ya fedha katika Halmashauri ya Mji Geita


Pia amemuagiza katibu Mkuu huyo  kufanya uchunguzi zaidi  kwa mwanasheria  na mwekahazina wa Halmashauri hiyo wakiwa ni washauri wakuu wa Mkurugenzi ni kwa jinsi gani waliweza kutimiza majukumu yao kikamilifu katika kushauri  kuhusu ununuzi wa gari hilo.  


Sambamba  na hilo  Waziri Jafo  amekiagiza Kitengo cha ukaguzi Ofisi ya Rais-TAMISEMI  kufanya uchunguzi  na ufuatiliaji kwa Halmashauri  nyingine zenye kutiliwa shaka kama zilienda kinyume  cha taratibu ya matumizi ya fedha.


Aidha,amemuagiza Katibu Mkuu kuunda timu itakayochunguza Ofisi ya Mkurugenzi, Manunuzi, Mwekahazina na Wakuu wa vitengo wote wa   Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda juu ya  tuhuma zinazotolewa na wananchi  kuhusu matumizi mabaya ya fedha katika Halmashauri hiyo,  ili endapoitabainika kuwa ni kweli hatua sitahiki zitachukuliwa kwa wahusika.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad