WAZIRI MHAGAMA: Wastaafu walipwe mafao kwa wakati kupunguza malalamiko.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 

Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa kufunga semina ya wajumbe wa Shirikisho la Mashirika  ya Hifadhi ya Jamii (TSSA) walipokutana tarehe 19 Desemba, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Gold Crest Jijini Mwanza.Mkutano ulihudhuriwa na Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi mbalimbali wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko hiyo.



Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini (TSSA) Bw. Meshack Bandawe,akizungumza kuhusu shirikisho la Mifuko hiyo wakati wa mkutano wao mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku Tatu mkoani Mwanza.



Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Mkurugenzi Mkuu wa NSSSF Bw. Hosea Kashimba.

Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Mwenyekiti wa Shirikisho la Mashirika ya Hifadhi ya Jamii (TSSA) Bw.William Erio mara baada ya kuhitimisha wa mafunzo kwa wajumbe wa Shirikisho hilo.



Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatulia hotuba ya Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.



Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Sekretarieti walioandaa semina hiyo iliyowakutanisha Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi mbalimbali wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko hiyo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

******************************************

Na. Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka mifuko ya Hifadhi ya jamii kulipa mafao ya wanachama wao kwa wakati ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima.

Ametoa kauli hiyo Desemba 18, 2020 alipokuwa akifunga semina ya siku tatu iliyolenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Shirikisho la Mashirika ya Hifadhi ya Jamii (TSSA) na kuhudhuriwa na  Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi mbalimbali wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko hiyo.

Waziri alieleza, upo umuhimu wa kila mfuko kuona tija ya kulipa wanachama wao kwa wakati ili kuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza kwa wale wenye sifa za kulipwa na kusaidia wanachama hao kukidhi mahitaji yao kwa wakati mwafaka.

 “Ni lazima kuhakikisha kuwa wanachama wanalipwa mafao yanayoendana na wakati ili kuwawezesha kukidhi matarajio yao bila kusahau wana mchango mkubwa katika mifuko yetu”. alieleza waziri

Alifafanua kuwa, amekuwa akipokea malalamiko mengi kwa wastaafu kuhusu ucheleweshwaji wa mafao yao, hivyo kuonesha viashiria vya udhaifu kiutendaji na kuzielekeza mamlaka husika kutatua changamoto hiyo kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu.

Aliongezea kuwa, mifuko inawajibu mkubwa wa kuhakikisha Waajiri wanaandikishwa na wanalipa michango kwa wakati.Idadi ya Waajiri ambao hawalipi michango imeongezeka hususan makampuni ya Ulinzi.

“Mifuko ipunguze usumbufu usikuwa wa lazima kwa wanachama hasa baada ya kustaafu na kudai mafao, kwa mfano mwanachama anastaafu akiwa na miaka 60 anaanza kudaiwa nyaraka ambazo aliwasilisha wakati anasajiliwa, kama kuna mabadiliko ya taarifa zinatakiwa zifanyiwe kazi na maafisa matekelezo kabla mwanachama kustaafu,”alisisitiza Waziri Mhagama  

Aidha alieleza kuwa Azma ya Serikali ni kuona Watanzania wote wenye uwezo wa kufanyakazi wana andikishwa katika Mifuko ya Pensheni maana  takwimu zinaonyesha bado kuna idadi kubwa ya wafanyakazi katika Sekta rasmi na isiyo Rasmi ambao bado hawajaandikishwa.

“Kwa kuangalia takwimu zilizopo, hadi sasa kuna jumla ya wafanyakazi walio andikishwa na kuchangia katika Mifuko  kwa idadi ndogo, mfano mfuko wa NSSF wapo  543,889 na PSSSF ni 627,097 ambapo idadi hiyo ni sawa na 4.3% ya nguvu kazi (Labour Force). Hivyo kazi kubwa inatakiwa kufanyika hususan katika Sekta isiyo rasmi,”alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Mashirika ya Hifadhi ya Jamii (TSSA) Bw.William Erio alipongeza jitihada za Waziri katika kuratibu na kusimamia shughuli za mifuko iliyochini ya ofisi yake na kuahidi kutekeleza maagizo yake aliyoyatoa pamoja na kuhakikisha wanakuwa na mikakati thabiti ya kushiriki katika miradi ya kimkakati ya Serikali ili kuwa na tija katika Taifa.

Aliongezea kuwa, wana lenga kuhakikisha wanaboresha huduma zao kwa wanachama na kuwafikia kwa wakati ili kuendelea kunufaika na uwepo wa mifuko nchini.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni haki yao..!!
    Ni WAJIBU WETU NA SIO HISANI, KUHAKIKISHA KWAMBA WANAPATA TENA KWA WAKATI..Mungu Baba mpe umuri mrefu huyu Jemedari ulituletea JPJM

    ReplyDelete
  2. Tena inasikitisha sana, MIMI ,Babu yangu Mzee Selemani amefanya kazi RAILWAY (EAR & TRC) Stesheni ya DODOMA

    TOKA SISI HATUJAZALIWA AMEFARIKI 1986 MPAKA HII LEO BIBI YANGU AMEZEEKA SANA
    HANA HATA BIMA WALA KUPATA MAFAO YA MAREHEMU MME WAKE. YUPO NYUMBANI HAPO EMAUSI AREA D. KIWANJA CHAKE SHULE YA DARUL NA BUNGE WAMEMCHUKULIA BILA MALIPO AJILI HAKUWA NA HATI MILIKI ATAYAJUAJE MTU SIEJUA KUSOMA WALA KUANDIKA..ANAMUAMINI MUNGU LAKINI SASA
    HII AWAMU YA KIPENZI CHETU JPM LABDA..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii, Taarifa ya Bi Mwanafatima Omari aliyekuwa na Shamba Mbugani, tunaielewa katika fukuza fukuza ya CDA Na ilikuwa inashughulikiwa na CDA. Na Mafao ya Mzee Selemani Athumani cheki iilikuwa inapitiwa Na TRC Makao Makuu kwa sasasina uhakika iko wapi miaka imeshakuwa mingi ila Wizara ziko Dodoma kwa sasa poleni kwa usumbufu. TUTALIANGALIA UPYA. mpitieni Mavunde na Mariamu Ditopile.

      Delete

Top Post Ad