WHO Yatuliza Hofu ya Virusi Vipya vya Corona

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna sababu ya watu kuwa na wasiwasi mkubwa kwa kuwa ni kawaida ya virusi kubadilika kunapotokea janga na kuongeza kuwa hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kwamba virusi vipya vya ugonjwa wa Covid-19 vinaweza kusababisha madhara zaidi kuliko vile vilivyokuwepo.

 

Virusi vipya vimegunduliwa Uingereza na baadaye Afrika Kusini na kuzua taharuki kubwa ulimwenguni kote, hali iliyosababisha mataifa kadhaa kuweka vizuizi vya usafiri kwa Uingereza na Afrika Kusini.

 

Wakati WHO ikitoa tamko hilo, mabalozi wa Umoja wa Ulaya (EU) wanakutana kwa dharura jijini Washington, Marekani, kuzungumzia jinsi ya kukabili aina mpya ya virusi hivyo vya corona.

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments