Yanga Nona Sana Wapindua Meza Kibabe, Waendeleza Rekodi


KLABU ya soka ya Yanga imeendelea ubabe wake ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kucheza jumla ya mechi 16 bila kupoteza kwa msimu wa 2020/21. 

Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji umekifanya kikosi hicho kijikite nafasi ya kwanza huku kikisepa na pointi tatu jumlajumla.


Licha ya kuanza kufungwa dakika ya nne na Seif Karihe walivuta subira mpaka dakika ya 27 ambapo walipachika bao la kuweka usawa kupitia kwa Lamine Moro.


Bao la pili lilipachikwa na ingizo jipya, Saido Ntibazokiza dakika ya 69 kwa mpira wa adhabu akiwa nje ya 18 ulioazama jumlajumla langoni.


Dakika ya 75 Dodoma Jiji wakiwa kwenye mapambano ya kuweka mzani sawa walikwaa kigingi cha tatu baada ya Saido kupiga faulo iliyokutana na nyota wao Bakari Mwamnyeto.


Mabeki wote wa kati wa Yanga leo wamefunga mabao na kufanya kikosi hicho kizamishe jahazi la Dodoma Jiji ambao walianza kwa kasi kipindi cha kwanza na kupoa kipindi cha pili.


Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 40 kibindoni huku ikiwa nafasi ya kwanza na kuwaacha wapinzani wao Simba walio nafasi ya pili kwa jumla ya pointi 8.


Simba ina pointi 32 imecheza mechi 14, watani hao wa jadi wamepoteza mechi mbili huku Yanga wakiwa hawajapoteza ndani ya ligi.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments