1/31/2021

50 Cent anataka kuingia ulingoni kuzichapa na Floyd Mayweather

 


50 Cent anataka kuingia ulingoni kuzichapa na Floyd Mayweather. Kwenye mahojiano yake kupitia V-103 "The Morning Culture", 50 Cent aliulizwa ni nani anataka kupigana naye kwenye pambano la masumbwi na hakusita kumtaja hasimu wake huyo wa muda mrefu.

"Nitapigana na Floyd. Lakini hofu yangu ipo kwenye uzito, sijui kama naweza kufanana naye." alisema rapa huyo na mfanyabiashara.

50 Cent aliwahi kuwa memba wa karibu na Mayweather na hata kuingia naye ulingoni siku ya pambano na Oscar De La Hoya. Wawili hao walikuja kupishana kutokana na kutokubaliana kibiashara.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger