1/22/2021

Afariki kwa Kukanyagwa na Treni Akidandia
MTU mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Noa amefariki dunia baada ya kukanyagwa na treni ya abiria akiidandia wakati ikiwa imeanza kuondoka katika stesheni ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

 

 

Noa anayedaiwa kuwa fundi ujenzi aliyekuwa akitoka Dar es Salaam kwenda Arusha amekanyagwa na treni wakati akijaribu kudandia treni hiyo iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Arusha leo Alhamis Januari 21, 2021.

 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa tukio hili lilitokea treni hiyo ilipofika stesheni ya Moshi.

 

Noa alishuka na kwenda kujisaidia na hivyo treni hiyo kumwacha na alipojaribu kuikimbiza ili apande kwenye behewa lake kwa bahati mbaya aliteleza na ikamkanyaga na kumkata vipande.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger