Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Aliyeuwa Wazazi Wake na Ndugu zake Kutoshtakiwa Tena..

 


Mvulana mwenye umri wa miaka 22 aliyekiri kuwauwa watu watano, akiwemo baba yake mzazi, mama yake na ndugu zake, hatashtakiwa baada ya Mahakama kutoa uamuzi wake.

 

Lawrence Waruinge mwanafunzi wa chuo kikuu aliyekiri kuwauwa ndugu zake hao wiki mbili zilizopita, huenda asishtakiwe tena na kuhukumiwa, baada ya Mahakama mjini Kiambu nchini Kenya kutoa uamuzi huo unao mzuia Lawrence kushtakiwa.


Ripoti kutoka idara ya upelelezi ilibaini kuwa Waruinge hana akili timamu baada ya kufanyiwa vipimo, hali ambayo imepelekea kesi yake kutoendelea na badala yake amepelekwa katika hospitali ya wagonjwa ya Madhare.

Join Our Telegram Group for Job Updates CLICK HERE


Upande wa mashtaka pia umemuachilia huru mpenzi wake Lawrence aliyeshtakiwa pia kushirikiana na Lawrence kutekeleza mauaji, na sasa yuko huru, akitakiwa kuwa shahidi wa upande wa mashtaka.


Waruinge sasa atatibiwa katika hospitali hiyo kwa siku 30 zaidi, ili kuona iwapo hali yake itaimarika.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments