Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Arsenal yavuliwa ubingwa wa FA


Klabu ya Arsenal imejikuta ikivuliwa ubingwa wa kombe la FA kwa mshangao baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Southampton, mchezo uliopigwa katika dimba la St Mary's.


Bao la Southampton lilikuwa ni la kujifungwa la mlinzi wa Arsenal , Gabriel ambaye alijikuta aukiuweka kimiani mpira wa krosi uliopigwa na Kyle Walker Peters dakika ya 24 ya mchezo.Lilikuwa ni bao la kwanza kwa Arsenal kuruhusu baada ya dakika 508 na pia kilikuwa kipigo cha kwanza kwa The Gunners baada ya michezo takribani 7 kucheza bila kupoteza.Arsenal ilikosa huduma ya mshambuliaji wake Pierre Emerick-Aubameyang na Emile Smith Rowe lakini ilimtumia Bukayo Saka katika kipindi cha pili cha mchezo huo.Akizungumzia kipigo hich, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ni bahati mbaya sana wameondolewa katika michuano hiyo kwakuwa walikuwa na matatizo ya kiufundi uwanjani hususan kipindi cha kwanza cha mchezo.Ni kwa mara ya kwanza Southampton inaitoa timu bingwa katika mashindano tangu wafanye hivyo mwaka 1902 walipoinyuka Tottenham Hotspurs, lakini pia ni kwa mara ya kwanza ndani ya misimu minne iliyopita, Arsenal wanaondolewa katika mashindano hayo.Watakatifu hao sasa watakabiliana na Wolves katika hatua inayofuata

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments