1/20/2021

Ashikiliwa na Polisi Akidaiwa Kumuua Mtoto wa Mumewe

 


Dar es Salaam. Jeshi la polisi Wilaya ya Kinondoni linamshikilia, Pendo Carlos kwa tuhuma za kumuua mtoto wa mumewe na kujaribu kuwaua watoto wengine wawili kwa kuwatumbukiza kwenye shimo la kuvuna maji ya mvua.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Januari 20, 2021 na kamanda wa polisi wilayani humo, Ramadhani Kingai katika mkutano wake na waandishi wa habari na kubainisha kuwa tukio hilo limetokea jana Januari 19, 2021 eneo la Tegeta A .

Amesema polisi walipokea taarifa kutoka kwa Roda Beda ambaye ni ndugu wa marehemu kwamba amepokea ujumbe wa mtuhumiwa unaosema, ‘mdogo wangu nimeamua kujiua kwa sababu ya kunyanyaswa na wake wenzangu.’

"Baada ya kupokea ujumbe huo ndugu wa mtuhumiwa akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliondoka na kuelekea nyumbani, alipofika alikuta mlango umefungwa na alipogonga geti ili afunguliwe hapakuwa na dalili za mtu kufungua ndipo alipofanya jitihada za kuvunja geti na kuingia ndani.” 

"Baada ya kuingia ndani alikuta mwili wa binti wa mume wa dada yake, Belinda Carlos (17) ukiwa chini na wakati akiendelea kuchunguza chanzo ndio aliposikia kelele za watoto zikitoka ndani ya shimo la kuvunia maji ya mvua. Aliomba msaada kwa majirani na walifanikiwa kuwatoa watoto wawili Bertha (4) na Brighton (6) wakiwa hai kutokana na shimo hilo kuwa na maji kidogo,” amesema kamanda huyo.


 Kamanda Kingai amesema baada ya mtuhumiwa kufanya tukio hilo aliondoka na kuelekea Sinza na alichukua chumba namba 111 kwenye hoteli ya  Movec na kunywa kitu kinachodhaniwa ni sumu kwa nia ya kutaka kujiua lakini wahudumu walimuokoa.


"Wahudumu baada ya kusikia akihangaika walimchukua na kumpeleka hospitali ya Sinza Palestina na alilazwa akiwa chini ya ulinzi wa polisi ila hali yake bado mbaya,” amesema.


Amesema mwili wa Brenda ulikutwa na mtandio shingoni na kulazwa sakafuni.


"Chanzo cha tukio hili inadaiwa ni mgogoro wa kifamilia, inadaiwa  mtuhumiwa ndio alisababisha kifo cha mumewe,  Carlos Myakunga (52) aliyefariki Mei, 2020 kwa maradhi,” amesema kamanda huyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger