Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Askofu Shoo amvaa meya aliyewavua watu barakoaMoshi. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu kuwaamuru wananchi waliokuwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kuvua barakoa.


Askofu Shoo, ambaye pia ni mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya kanisa hilo, alisema kitendo cha meya huyo kuwalazimisha wananchi wanne kuvua barakoa ni kukosa hekima na uwajibikaji wa kiwango cha juu kama kiongozi wa kisiasa.


“Itoshe tu kusema nimesikitishwa sana na kitendo cha huyu meya, kuwalazimisha watu kuvua barakoa, ni kukosa hekina na uwajibikaji kwa kiwango cha juu,” alisema Askofu Shoo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kujikinga.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments