Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Baada ya miaka 8 Man United yaonja mafanikio


Klabu ya soka ya Manchester United ya nchini England, imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa ligi kuu nchini humo uliopigwa usiku wa kuamkia leo Januari 13, 2021.

 

Baada ya ushindi huo ambao goli pekee lilifungwa na Paul Pogba dakika ya 71, Manchester United sasa imefikisha pointi 37 na kukaa juu ya  msimamo ikiwazidi Liverpool ambao wana pointi 33, baada ya timu zote mbili kucheza mechi 17 mpaka sasa.


Hii ni mara ya kwanza Manchester United inaongoza ligi kuu ya England baada ya kuwa imecheza mechi nyingi (17), ambapo mara ya mwisho kuongoza ligi baada ya mechi nyingi ilikuwa ni siku ya mwisho ya msimu wa 2012-13 walipotwaa ubingwa chini ya Sir Alex Ferguson.
Wachezaji wa Manchester United wakishangilia goli


Hata hivyo mbio za ubingwa ndio kwana mbichi kutokana na ushindani ambao upo msimu huu ambapo vilabu vingi vimekuwa vikisuasua.


Katika ligi ya msimu huu nchini England  karibu timu sita zimeshakaa kwenye usukani wa ligi ya nchi hio mpaka sasa ambazo ni  Manchester United, Southampton, Aston Villa, Liverpool, Tottenham na Everton

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments