Baba Levo: Natamani nife wa kwanza kabla ya Diamond, akitaka lolote ntamfanyia. Wadau wamfananisha Baba Levo na Gigy Money

advertise here

Msanii Baba Levo ameweka wazi kuwa anatamani Mungu amchukue hata leo ili watoto wake walelewe na Diamond.


Baba Levo amesema hayo akieleza hisia zake baada ya Diamond kumlipia ada za watoto wake wawili wanao soma TUSIME SEC.


Baba Levo anasema anatamani Mungu amchukue hata leo kabla hajamchukua Diamond kwani Diamond ni muhimu hapa duniani kuliko yeye .... napia amesema yuko tayari kumfanyia chochote Diamond akimwambia...maana ni mtu muhimu sana kwake.


Hata hivyo wadau wengi wamekuwa wakimuona Baba Levo kama ni mtu aliye na matatizo ya akili hivi karibuni kiasi ambacho utofauti wake na Msanii Gigy Money ni mdogo sana na wengine wamekwenda mbali zaidi kumthadharisha Diamond kuwa makini na watu ya aina ya Gigy na Baba Levo ambao wanaweza kumponza zaidi kwani wamekuwa wakiropoka sana bila kujali wako watu na wana muingiza kwenye gharama sana.


Hata hivyo wadau wamemuomba Diamond kumpatia Baba Levo Daktari wa Magonjwa ya akili.

Wasalaam

By Ruttashobolwa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE