Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Baba Mbaroni kwa Kubaka, Kumpa Ujauzito Binti Yake!
KIJANA mmoja mkazi wa kijiji cha Igunila kata ya Ziba wilayani Igunga mkoani Tabora, Sharif Idd Maganga (28) amekamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa katika mahakama ya wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya kumbaka binti wa miaka 14 na kumsababishia ujauzito.

 

Awali, Mwendesha mashitaka wa polisi wilaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba aliiambia mahakama mbele ya hakimu wa wilaya ya Igunga Eddah Kahindi kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 130 (1) (2) (e) na 131 (1) kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019.

 

Mwendesha mashitaka huyo alisema mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo katika tarehe tofauti ya Januari na Agosti mwaka jana kwa muda tofauti katika kijiji cha Igunila kata ziba.

 

“Mshitakiwa Sharif Idd alikuwa akifanya mapenzi na binti huyo ambaye ni mtoto wake wa kambo mkazi wa kijiji hicho cha Igunila ambaye jina limehifadhiwa na kumsabishia ujauzito,”.

 

Hata hivyo, baada ya kusomewa shitaka mshitakiwa alikana shitaka ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 19 mwaka huu itakapotajwa na mshitakiwa amepelekwa mahabusu.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments