Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Babu Tale "Mke Wangu Aliniambia Nisioe"


 Meneja wa WCB, Mh. Hamisi Taletale @babutale, ambaye alifiwa na mkewe Shamsa Kombo 'Shammy' Juni 26, 2020, afunguka mazito kuhusiana na Marehemu mke wake kwenye mahojiano na mtangazaji Salama Jabir kwenye kipindi chake cha SalamaNa.


"Marehemu mke wangu tulifahamiana Magomeni Kota kwa sababu na yeye alikuwa anaishi pale, nilimtongoza mwaka mzima hajanikubali. Enzi hizo nilikuwa mtu flani rafu halafu yeye ana mambo ya kizungu” ameeleza Babu Tale.


“Mke wangu aliniambia nisioe, nakumbuka hiyo siku nimeshinda naye Muhimbili, akaniambia nimechoka kuishi hii hali, akanishika mkono kuniambia mimi naondoka, lea watoto lakini usioe, usioe, usioe”.


#BabuTale aliendelea, “Kinachoniliza ni kupoteza mtu ambaye angeweza kuniongoza kwa vitu vingine, nimepata uongozi lakini yule aliyetakiwa kula good time hayupo”.


Marehemu #Shammy enzi za uhai wake alifahamika zaidi kutokana na asasi yake aliyoimiliki ya 'Nasimama Nao' iliyokuwa ikiwasaidia kina mama na mpaka mauti yalipomkuta. Shmmy ameacha watoto watatu, wawili wa kiume na mmoja wa kike.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments