Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Bernad Morrison Amkimbiza Carlinhos Bongo
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, amewakimbiza vibaya mastaa wa Yanga kwa kumiliki ndinga yenye thamani kubwa akiwemo Carlos Carlinhos.


Morrison raia wa Ghana, anamiliki gari aina ya Nissan Fuga 50GT ya mwaka 2013 yenye thamani ya Sh milioni 63, huku Muangola, Carlinhos akimiliki gari aina ya Subaru Impreza WRX Hatchback ya mwaka 2011 yenye thamani ya Sh milioni 32.

Hata hivyo, licha ya Morrison na Carlinhos kumiliki ndinga hizo, bado hawajatosha kukimbiza katika soka la Bongo kwani wameachwa mbali na kiungo wa Azam FC, Ally Niyonzima anayetembelea ndiga ya thamani kuliko wachezaji wote kwa sasa hapa nchini.


Kiungo huyo mwenye uraia wa Rwanda ambaye alijiunga na Azam msimu huu akitokea Rayon, gari yake ni BMW 4 Series Gran Coupe ya mwaka 2014 yenye thamani ya Sh milioni 80.

Mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa raia wa Zambia, ni mchezaji wa tatu kwa kumiliki ndinga kali ambapo jamaa huyo anayo Mercedes Benz E Class yenye thamani ya Sh milioni 52.
Carlinhos anakuwa mchezaji wa nne kwa kumiliki ndinga kali, huku nafasi ya tano ikishikiliwa na beki mpya wa Polisi Tanzania, Kelvin Yondani ambaye anamiliki ndiga aina ya Suzuki Grand Vitara ya mwaka 2014 yenye thamani ya Sh milioni 28.


Wachezaji wa Simba, Jonas Mkude na John Bocco, kila mmoja anamiliki gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya Sh milioni 27.

Beki wa Azam FC, Aggrey Morris, anafuatia kwenye orodha hii akiwa anamiliki ndiga aina ya Toyota Rav 4 ya mwaka 2013 yenye thamani ya Sh milioni 22.Nyota wa Simba, Ibrahim Ajib, Gadiel Michael, Hassan Dilunga, Mohammed Hussein, Clatous Chama na Adam Salamba wa Namungo, kila mmoja anamiliki ndinga aina ya Toyota Crown yenye thamani ya Sh milioni 19.


Shomari Kapombe, Kennedy Juma na Beno Kakolanya wanaoitumikia Simba, kila mmoja anamiliki ndiga aina ya Toyota Mark X yenye thamani ya Sh milioni 17, huku kipa wa Yanga, Metacha Mnata akimiliki Toyota Allion yenye thamani ya Sh milioni 15.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments