Bilionea Dangote Apoteza Tril. 2, Utajiri Waporomoka
MWENYEKITI wa kampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote,  amepoteza kiasi cha Dola milioni 900 katika hisa nchini Nigeria ambazo ni  sawa na Sh. trillioni mbili za Tanzania, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bloomberg.

 

Kwa mujibu wa Bloomberg, ambalo huripoti kuhusu watu 500 tajiri zaidi duniani, mapato ya Dangote yalishuka kutoka dola bilioni 18.4 siku ya Alhamisi hadi dola bilioni 17.5 siku ya Ijumaa.  Kwa mujibu wa gazeti la Punch hali hiyo imemfanya kushuka hadi mtu wa 106 katika orodha ya watu tajiri zaidi duniani.

 

Hata hivyo,  Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika na mtu mweusi tajiri zaidi duniani.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments