Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Bingwa wa Simba Super Cup Kulamba Mil. 15
KLABU ya Simba imeweka wazi zawadi atakazopata bingwa wa michuano ya Simba Super Cup iliyoanza Januari 27, 2021 ambazo ni fedha taslimu shilingi milioni 15, kikombe na medali.

 

Taarifa hiyo imetolewa leo kupitia kwa Ofisa Habari wa timu  hiyo, Haji Manara, ambaye pia amesema baada ya mchezo wa mwisho kutakuwa na tafrija (after party) ambayo itafanyika ‘Kidimbwi Beach’ jijini Dar es Salaam.Katika hatua nyingine,  Manara amemtangaza msanii wa Bongo Fleva Zuchu kuwa mtumbuizaji katika mchezo wa mwisho wa michuano hiyo utakaopigwa Jumapili, Januari 31, 2021 kati ya Simba vs TP Mazembe.

 

“Mashabiki mfike mapema uwanjani na mjifunze namna ya kucheza sukari,” amesisitiza Zuchu ambaye pia amemtaja golikipa Aishi Manula kuwa ndiye mchezaji anayemvutia zaidi kutoka kwenye kikosi cha Simba.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments