Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Bobi Wine Apinga Matokeo Uchaguzi Mkuu Uganda

MGOMBEA wa upinzani nchini Uganda katika nafasi ya urais, Bobi Wine, leo Januari 15, 2021,  amepinga matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa hadi sasa na kujitaja binafsi kama rais mteule, licha ya tume ya uchaguzi kusema kuwa siyo kura zote zilizokwishahesabiwa.

Bobi Wine anadai uchaguzi wa Alhamisi ulitawaliwa na wizi mbaya zaidi wa kura kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Uganda, lakini hakutoa ushahidi wowote kuhusu madai yake.

Ametangaza kuwa mapambano ndiyo kwanza yameanza.

Mgombea huyo jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anasema kuwa atazungumza na waandishi wa habari saa chache zijazo juu ya kitakachofuatia.

Matokeo ya awali yanayotolewa na Tume ya Uchaguzi yanaonyesha Rais Yoweri Museveni anaongoza kwa zaidi ya asilimia 60.

Wakati huohuo, wanajeshi wameizingira nyumba ya Bobi Wine.

NECTA Watangaza MATOKEO ya ‘FORM’ 4, 2 na DARASA LA 4, Mwanafunzi ALIYEONGOZA KITAIFA..
 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

2 Comments

 1. Huyu nae Ti lampu Mwingine. Kama Tundu Bovu vile. Pipo Pwaa..Pwa..PWAAAAA

  Mwenzako Kibeko kaenda kwao Ubelijiji wewe utaenda kupiga disco ya kolabo na nguli wa hip hop Mr. HamoRapa wapi? Sina uhakika kama ameikubali kolabo

  ReplyDelete
 2. Maandamano ya siyo na kikomo,ndio mazungumzo na mafundisho ya hawa VIBARAKA
  wanayo fundishwa na Low Bati Ansata Damu.

  Waganda wamelistukia hilo. Hawamwagi Damu na kuvunja Amani.

  Tafuta mchango wa auli kwenda Ubelijiji.

  ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)