Breaking: Bunge Lathibitisha Biden Rais Mteule Marekani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





BUNGE  la Congress nchini Marekani limemuidhinisha Joe Biden kuwa rais mteule wa Marekani na Kamala Hariss kuwa makamu wa rais.

 

Bunge hilo liliwaidhinisha wawili hao kwa kura 282 huku wabunge 138 wakipiga kura ya kupinga matokeo ya jimbo la Pennsylvania. Bunge la seneti lilikataa pingamizi hilo.

 

Kura za wajumbe zilithibtishwa baada ya mabunge yote mawili, lile la uwakilishi na lile la seneti kukataa pingamizi kuhusu kura zilizopigwa katika vituo vya jimbo la Pennsylvania na Arizona.

 

Shughuli za bunge zilikatizwa siku ya Jumatano wakati wafuasi waTrump walipovamia jumba la Capitol Hill. Shughuli baadaye zilirejea na kuendelea usiku kucha baada ya waandamanji hao kutolewa.

 

Bunge la uwakilishi pamoja na lile la Seneti litaendelea kuhesabu kura za wajumbe zilizosalia ili kumuidhinisha Joe Biden kuwa rais mtarajiwa wa Marekani.

 

Makamu wa Rais, Mike Pence, alitoa tangazo hilo pamoja na Spika wa bunge la uwakilishi, Nancy Pelosi, katika mkutano wa pamoja wa mabunge yote.
 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad